Kizuizi cha uwajibikaji

1 Mada ya kanuni za matumizi; kiwango cha kutumiwa
1.1. Kanuni zifuatazo zinatawala matumizi ya michezo ya mtandaoni ambayo imetolewa na Gameforge katika kurasa za nyavuti zake.\t\tKwa kusajili au kuingia kwenye kiingilio cha ukurasa wa Gameforge, www.mmogame.com, watumiaji wanaingia kwenye mkataba huu wa mtumiaji na Gameforge 4D GmbH kuhusiana na michezo ya mtandaoni ya wateja-yani, michezo ile inayohitaji kupakuliwa na mteja. Katika hali hizi, Gameforge Productions GmbH inachukuwa nafasi ya wakala halisi wa Gameforge 4D GmbH kwa mujibu wa usajili na kuingia kwenye kiingilio cha ukurasa wa Gameforge.
1.2. Kanuni hizi za matumizi zinasawazisha kabisa matoleo ya kitambo ya kanuni za matumizi ya Gameforge.
1.3. Gameforge inatoa michezo ya mtandaoni pamoja na huduma nyingine ndani ya mpangilio wa uwezo wake wa kiufundi na kiutenda kazi huku ikiwa na uwepo wa wastani wa kila mwaka wa 98.0%. Vipindi vya muda wa kukatiza michezo hii ya mtandaoni pamoja na kutolewa kwa huduma nyingine havijahesabiwa hapo au kuathiriwa kwa sababu ya sababu zenye nguvu za kiufundi au kazi ya ukarabati inayohitajika bila ya Gameforge kutoa fidia ili kuenda sambamba na kauli za mkataba huu.
1.4. Gameforge inaunda, inadurusu na pia vilevile kutumia michezo yake ya mtandaoni na huduma nyingine kila wakati. Kwa jinsi inavyohitajika, watumiaji wanaweza kushiriki tu katka michezo na huduma za mitandaoni kwenye matoleo yao ya sasa.
1.5. Michezo ya mtandaoni na huduma nyingine zinazotolewa na Gameforge zimenuiwa kutoa burudani pekee na haifai kutumiwa katika kutoa tuzo ya kifedha au sababu ya kibiashara.
1.6. Ni jukumu la mtumizi kuhakikisha kwamba kiinieroro na kiinigumu anachotumia kinakubalika na kinafaa.
1.7. Kwa kuongezea kanuni hizi za matumizi, sheria zilizopo katika kila mchezo wa mtandaoni zinatumika, kama zipo. Endapo patatokea mgongano wowote kati ya kanuni hizi za matumizi na sheria za mchezo, kanuni hizo zitatumika.Katika kila michezo ya mtandaoni, pamoja na lakini michezo ambayo haijazuiliwa kutofautiana na/au viungo vilivyomo ndani yake, na kuongezea huduma za kibinafsi kwenye kurasa za nyavuti za Gameforge ambazo zitaangaziwa na kanuni maalumu za matumizi, na kuarifiwa kwa watumiaji kabla ya matumizi. Katika baadhi ya michezo na huduma za mtandaoni, watumiaji wanayo fursa ya kutumia huduma za watoaji huduma wa Gameforge. Katika muktadha huu mkataba mwingine tofauti kati ya mtumiaji na mtoaji huduma husika wa Gameforge, hutumika ambapo mtumiaji anaarifiwa kwa njia inayofaa kabla ya hitimisho ya mkataba kufikiwa.
1.8. Kutumiwa kwa sheria za mtumiaji au kanuni na masharti ambayo yataenda mbali na kanuni hizi za matumizi kutakuwapo tu , endapo kampuni ya Gameforge itakubali mapema utumikaji wake kwa njia ya kuandika.
1.9. Kauli nyingine au masharti na kanuni za mtumiaji zitatumika tu, endapo kampuni ya Gameforge itakubali mapema utumikaji wake kwa njia ya kuandika.
2 Hitimisho
2.1. Usajili wa watumiaji ni lazima ili watumie michezo ya mtandaoni na huduma nyinginezo zinazotolewa na kampuni ya Gameforge.
2.2. Usajili umehifadhiwa watu binafsi,watu binafsi tu ndio wanaokubaliwa kuwa watumiaji halali (hakuna makundi, familia, watu wanaoishi pamoja, n.k.). Mradi tu watumiaji wawe wachanga, kule kutuma kwao kwa ombi la usajili, kutatokea tu endapo idhini kamilifu ya mwakilishi wake wa kisheria ipo.
2.3. Wakati wa usajili, watumiaji watahitajika kutoa jina la mchezaji na baruameme iliyosajiliwa kwa jina lao. Watumiaji hawahitajiwi kutumia jina la kuchezea ambalo ni chaguo lao. Majina ya kuchezea hayafai kuingilia haki za watu wengine au kuudhi.Vilevile watumiaji hawaruhusiwi kuchagua baruameme au wavuti kuwa jina la kuchezea. Watumiaji wahakikishe kwamba taarifa walizotoa wakati wa usajili kwenye kampuni ya Gameforge, ni za kweli na kamilifu.
2.4. Usajili wa watumiaji lazima uwe wa mtu binafsi; hawawezi kusajiliwa na mtu mwingine, pamoja na wale ambao hufanya usajili wa watu binafsi walio na huduma mbalimbali za mawasilano, lakini si hao tu, kwa njia ya kibiashara (huduma za usajili).
2.5. Usajili mbalimbali unaidhinishiwa kwenye kiingilio cha kampuni ya Gameforge na kwenye nyavuti za michezo ya mtandaoni kupitia kwa thibitisho la baruameme ambalo linawapa watumiaji kiungo cha uwezeshaji. Katika hali hizi, kampuni ya Gameforge huwezesha akaunti ya mtumiaji/mchezaji endapo na wakati ambao kiungo cha uwezeshaji kinabonyezwa. Kwa uwezeshwaji wa akaunti au kuchukuliwa kwa mtumiaji naGameforge, mkataba wa leseni ulio na muda usiojulikana kati ya Gameforge na mtumiaji hufanywa kwa kurejelea kanuni hizi. Katika kesi mbalimbali, mchakato wa usajili hubadilika kiasi nje ya utaratibu uliotajwa hapo juu, ambapo mtumiaji huarifiwa kwa njia inayofaa.
2.6. Baada ya watumiaji kufanya usajili kamilifu, wanaweza kuziunda na kuzisimamia akaunti zao za mtumiaji, pekee yao. Wanaweza kuzifungua akaunti za mtumiaji katika ukurasa wa Gameforge wa kiingilio pamoja na kwenye ukurasa wowote wa mchezo wa mtandaoni. Akaunti ya mtumiaji iliyoundwa kwenye ukurasa wa Gameforge wa kiingilio inaweza pia kutumika katika michezo mingine yote ya mtandaoni ambayo Gameforge itaweka kwenye kiingiliio chake kwa njia ya viungo. Hata hivyo, akaunti za mtumiaji zilizoundwa kwenye ukurasa wa mchezo wa mtandaoni huenda zisitumike katika michezo mingine ya mtandaoni.
2.7. Akaunti za mtumiaji haziwezi kuhamishwa bila ya idhini halisi kutoka kwenye kampuni ya Gameforge.
2.8. Watumiaji hawaruhusiwi kusajiliwa na kuchukuliwa na hawawezi kusajiliwa zaidi ya mara moja. (k.m.f.,Dunia,Ulimwengu, n.k.) kwenye michezo ya kusakura. Kama mtumiaji tayari amesajiliwa katika raundi moja, yeye anazuiliwa kusajiliwa katika raundi hiyo kwa muda uliowekwa katika usajili wake (k.m.f., kwa kuingiza taarifa nyingine za kibinafsi au zilizotofautiana kidogo na za awali.
3. Ufafanuzi wa ufutiliaji mbali
Haki ya kufutilia mbali
Unaweza kufutilia mbali mkataba wako kwa maandishi ndani ya wiki mbili bila kutoa sababu. (k.m.f. barua, faksi,
baruameme). Kipindi hicho cha wiki mbili kinaanza kuanzia wakati ambao ufafanuzi huu unapokelewa kwa maandishi
na si kabla ya hitimisho ya akaunti au utoshelevu wa majukumu yetu ya ufafanuzi uliomo kwenye mkataba ndani ya
kifungo cha § 312c (2) katika msimbo wa kiraia wa Ujerumani (Bürgerliches Gesetzbuch ) kwa ushirikiano na § 1, (1),
(2) na (4) ya amri ya ufafanuzi wa BGB (BGB-Info V) pamoja na majukumu yetu yaliyomo kwenye mkataba § 312e, (1)
sentensi ya 1 ya BGB kwa ushirikiano na § 3 BGB-InfoV. Ili kuweza kutosheleza, arifa za ufutiliaji mbali zinahitajika
kutumwa mapema kwa Gameforge Productions GmbH, Albert-Nestler-Strasse 8, 76131 Karlsruhe
Athari za ufutiliaji mbali
Kwenye uwezekano wa ufutiliaji mbali kamilifu, huduma kama hizi kwa jisi zilivyopokelewa na faida kama hizi (k.m.f.,
riba) kama zitakavyokuwa zimetolewa kutoka mojawapo ya pande, zitaweza kurudishwa nyuma na/au kurejesha.
Endapo hutaweza kuzirudisha nyuma na/au kuzirejesha huduma zote zile ulizopokea kutoka kwetu katika hali ambayo
zilitolewa, basi huenda ukatudai fidia kama inavyofaa. Jukumu lako kurudisha malipo linafaa kutiliwa maanani ndani
ya siku 30 kuanzia tarehe ambayo arifa yako ilitumwa au, kwetu sisi, tarehe ambayo ilipokelewa.
Kanuni maalumu
Haki yako ya ufutiliaji mbali itaisha kwa ghafla endapo (i) Kampuni ya Gameforge imeanza tayari kutoa huduma kwa I dhini yako kamilifu au (ii) kama wewe umejitakia hivyo mwenyewe kwa kuanzisha huduma kama hiyo kabla ya tarehe
ya mwisho ya ufutiliaji mbali huo. Hali hii inafaaa ichukuliwe kuwa hivyo endapo ulishirirki katika mchezo huo wa
mtandaoni au ulifurahia huduma nyinginezo.
Mwisho wa ufafanuzi wa ufutiliaji mbali
4 Majukumu ya mtumiaji
4.1. Deta ya mtumiaji
Mtumiaji anakubali kuarifu kampuni ya Gameforge kuhusu mabadiliko yote yatakayotokea kwenye siku za usoni yanayohusiana na taarifa ambayo walitoa kama sehemu ya mchakato wa usajili pamoja na mabadiliko kwenye anwani zao za baruameme, lakini si tu katika mabadiliko hayo pekee. Watumiaji wanahitajika kuthibitishia kampuni ya Gameforge uhakika wa taarifa zao,pindi tu watakapoulizwa.
4.2 Deta ya kufungua, utambulisho, manenosiri
4.2.1. Watumiaji wanahitajika kuhifadhi taarifa yao yote ya kufungua,utambulisho na manenosiri faraghani kabisa.Watumiaji hawafai kuingiza deta ya kufungua katika kurasa za mtandaoni ambazo hazisimamiwi na kampuni ya Gameforge.
4.2.2. Istilahi “deta-ya kufungua” na “utambulisho na manenosiri” zinarejelea mseto wa herufi na/au alama na/au nambari ambazo hutumika kuhalalisha watumiaji na kumzuia mtu mwingine kutumia. Manenosiri hayafai kuwa sawa na jina la mchezaji na kwa kiasi fulani ni mseto wa nambari na herufi.
4.2.3. Watumiaji wanahitajika kulinda deta yao yote ya kufungua, utambulisho na manenosiri dhidi ya watu wengine wanaoweza kuifikia.
4.2.4. Kwenye tukio la watumiaji kuwa na sababu ya kuamini kwamba watu wengine wamechukua taarifa hii, au huenda Wamechukua deta aina hii bila idhini, wanahitajika kuarifu mara moja kampuni ya Gameforge ili kubadilisha deta yao au kushauri kampuni ya Gameforgekuibadilisha. Katika tukio hili au wakati ambao kampuni ya Gameforge itakuwa na idhibati ya matumizi mabaya ya deta, kampuni ya Gameforge ina haki ya kuzuia akaunti hii kufikiwa kwa muda. Mtumiaji ataruhusiwa tu kutumia tena baada ya shuku ya matumizi mabaya ya deta hiyo kuondolewa.
4.2.5. Watumiaji kwa vyovyote vile hawaruhusiwi kutumia deta ya watumiaji wengine ili kuingia kwenye akaunti zao isipokuwa pale ambapo sheria za mchezo zinaztoa maelekezo maalum ya kufanya hivyo.
4.3 Matumizi ya kurasa na yaliyomo kwenye tovuti za kampuni yaGameforge.
4.3.1. Tovuti ya Gameforge hutoa makala mbalimbali ambayo yamelindwa kwa manufaa ya Gameforge au makundi mengine yaliyo na nembo, hakimiliki, na sheria nyingine. Kanuni hizi za matumizi zisipoeleza vinginevyo, basi watumiaji hawahitajiki kuchakata, kunakili, kusambaza, kuchapisha, au kutumia katika matangazo au katika makusudio ya utoaji zaidi wa huduma kwenye tovuti za Gameforge au makala yoyote yaliyotolewa hapo. Unakili unaruhusiwa tu kwa sababu ya sababu za kiufundi na makusudio ya kusakura. Unakili wa kuendelea ni wa sababu za kibinafsi tu. Taarifa ya hakimiliki na nembo haifai kubadilishwa au kubatilishwa au kuondolewa.
4.3.2. “Yaliyomo” linarejelea deta zote, taswira, matini, michoro, muziki, sauti, msururu wa sauti, video, programu, misimbo ya kiinieroro na taarifa nyingine ambazo zinatolewa na kampuni ya Gameforge kwenye tovuti yake, pamoja na huduma zinazotolewa ili kupakua, lakini si katika huduma hizi pekee.
4.3.3. Watumiaji anahitajika kuepukana na (i)kuchukua hatua yoyote ambayo itahatarisha au kuhitilafiana na ufanyaji kazi bora wa tovuti ya Gameforge au huduma zozote zinazotolewa hapo, na (ii) kufikia deta ambayo mtumiaji haruhusiwi kufikia bila idhini. Makala hayo yaliyomo yanaweza kuonekana tu katika njia ambayo inakubalika na kufurahia kwa tovuti ya Gameforge na yaliyomo, na watumiaji wengine. Deta au kiinieroro ambavyo vinaweza kuathiri kiinieroro au kiinigumu cha mpokeaji havifai kusambazwa.
4.3.4. Matumizi ya tovuti ya Gameforge kwa manufaa ya kibiashara pamoja na matangazo ya biashara, lakini si hayo tu, yatategemea idhini ya moja kwa moja kwa maandishi kutoka katika kampuni ya Gameforge kabla ya matumizi hayo.
4.3.5. Watumiaji hawana haki ya kuchapisha makala yaliyomo katika tovuti ya Gameforge.
4.3.6. Tovuti ya Gameforge huenda isifikiwe kwa kutumia huduma ya uanonimisheni ambayo inaficha anwani ya kweli ya IP ya mtumiaji.
4.4. Viungo
Vinaruhusiwa kuanzisha kiungo kwenye tovuti ya Gameforge mradi tu viungo vinatoa huduma ya marejeleo-mseto pekee. Gameforge inayo haki ya kutupilia mbali idhini hii. Hata hivyo haviruhusiwi kuhusisha au kuwakilisha tovuti ya Gameforge au makala yaliyomo kwenye fremu kwa kutumia kiungo cha kipekee.
4.5. Matumizi ya kiinierero cha mteja
Kwa mujibu wa huduma zinazozotolewa (pamoja na michezo), ambazo zinahitaji kuingizwa mapema kwa kiinieroro cha mteja kabla ya kutumiwa. Gameforge inawapa watumiaji haki batili(rahisi) kuingiza na kutumia kiinierero cha mteja kama hicho kwa muda ambao watumiaji hao watakuwa wamesajiliwa na Gameforge. Watumiaji wanaruhusiwa kunakili kiinieroro cha mteja kwa kiasi tu ambacho kitahitajia katika matumizi ya utoaji huduma huo. Kiinieroro cha mteja hakifai kutumiwa kwa sababu yoyote ya biashara. Sheria inayohusika isiposema hivyo, basi kiinierero cha mteja hakifai kubadilishwa, msimbo wa programu uliotolewa haufai kutafsiriwa upya hadi kwenye misimbo mingine. (upanguaji) na hatua mbalimbali za utayarishaji wa kinieroro hazifai kurejelewa tena(uhandisi rejelezi)
5 Kanuni maalumu kwa matumizi ya michezo ya mtandaoni
5.1. Watumiaji wamezuiliwa kuwa na akaunti moja ya mtumiaji (k.m.f.,Dunia,Ulimwengu, n.k.) isipokuwa tu sheria za mchezo zikiruhusu. Matumizi ya akaunti nyingi za mtumiaji hayaruhusiwi na Gameforge huenda, kwa chaguo lake, ikafuta au kuzuia wakati wowote akaunti nyingi za mtumiaji.
5.2. Watumiaji wamepigwa marufuku kutumia mfumo wowote utakaoingiliana au kuhitilafiana na michezo ya mitandaoni. Haswa, watumiaji hawaruhusiwi kutumia mbinu, njia au kiinieroro ambacho kinaweza kuhitilafiana na utendakazi au mkondo wa mchezo. Vilevile, watumiaji wasitumie mbinu ambazo zitasababisha uzito katika uwezo wa kiufundi kwa kiwango kilichokithiri au kisichofikirika. Watumiaji hawaruhusiwi kuzuia, kuandika upya au kuboresha makala yaliyomo na yaliyotolewa na msimamizi wa mchezo au watumiaji hao kuhitilafiana na michezo ya mtandaoni.
5.3. Watumiaji pia wamepigwa marufuku kuifikia michezo ya mtandaoni (pamoja na ukurasa wowote wa tovuti) kutumia programu nyingine mbali na kisakuzi cha wavuti au programu ya mteja ambayo imetolewa.Hii huwa kweli katika vidude viitwavyo kwa jina maarufu bots na zana nyingine ambazo zimenuiwa kusawazisha au kubadilisha sura ya wavuti. Nyingine zilizopigwa marufuku pia ni miswada na programu zilizo atomatiki kwa ukamilifu au kwa kiasi fulani na ambazo zinampa mtumiaji nguvu zaidi kuliko watumiaji wengine. Hii ni pamoja na majukumu ya kuchangamsha-kiatomatiki na mifumo mingine ya ndani kwa ndani ya kisakuzi ya wavuti pale ambapo operesheni za kiatomatiki zinahusika.
5.4. Watumiaji kwa hali yoyote ile hawaruhusiwi
a) \tkuunda au kutumia uwongo, udanganyifu na/au utapeli au kutumia kiinieroro kingine na hivyo basi kubadilisha hali ya kucheza ya wachezaji kwenye mchezo wa mtandaoni;
b) \tkutumia kiinieroro kwa sababu ya uundaji wa deta kama si “kudaka” au “kukusanya” inayohusiana na michezo ya mtandaoni;
c) \tkununua au kuuza kwa kutumia hela “halisi”, kubadilishana vifaa au kuvitumia vifaa kama hivyo nje ya michezo ya mtandaoni kama hiyo, na ambavyo vinatumiwa kwenye michezo ya mtandaoni.
Hii inahusisha kwa njia ya uepukano wote, hatua kama hizo au hatua zinazolingana katika athari ambazo zinaorodheshwa katika marufuku hayo yaliyotajwa.
5.5. Matumizi ya zana katika uzuiliaji wa matangazo hayaruhusiwi. Kwa sababu hii, hakuna uzito endapo matangazo maalumu ya biashara yatazuiliwa au vichipukizi maarufu yaani Pop-Ups kuzuiliwa au visakuzi vinavyorejelea matinikutumiwa ili kuzuia matangazo kuonekana.
5.6. Watumiaji wataruhusiwa tu kuingia kwenye akaunti kupitia kwenye ukurasa wa kuanzia katika mchezo huo au katika kiingilio cha ukurasa wa Gameforge. Ufunguaji wa kiatomatiki wa akaunti za mtumiaji hautakikani licha ya ukurasa wa kuanzia kuonekana.
5.7. Haki zote za vifaa vya mtandaoni ambavyo vimetolewa katika michezo ya mtandaoni dhidi ya ada inaenda katika kufaidi kwa kipekee kwa kampuni ya Gameforge na/au watoaji huduma wa Gameforge waliohalalishwa. Hali hiyo ni kweli pia katika vifaa vya mtandaoni vilivyoundwa na watumiaji, ambao wanapatia Gameforge,kote duniani, siku zote na bila kizuizi chochote, haki kamilifu ya kutumia kwa faida vifaa vya mtandaoni kama hivi, ambayo inahusisha unakili wavyo, usambazaji na uundaji. Watumiaji wanapokea tu haki ya muda ya matumizi ya faida katika vifaa kama hivi, na ambayo yamezuiliwa ndani ya kanuni ya mkataba.
6 Kanuni maalumu kwa matumizi ya hali za mawasiliano ( k.m.f., midahalo ya mazungumzo, kusogoa, michango) kuhusu tovuti ya Gameforge.
6.1. Gameforge inaweza kutoa, lakini watumiaji hawana lazima ya kupata, hali mbalimbali za mawasiliano kama vile midahalo ya mazungumzo, kusogoa, blogi, vitabu vya wageni pamoja na michango ya kazi) ili watumiaji waweze kuchapisha makala yao wenyewe na kuchangia kwenye tovuti ya Gameforge.Watumiaji wanaruhusiwa kutumia vizuri nafasi kama hizi kwa kiasi ambacho bado zipo.Gameforge inasimamia tu mabadilishano ya taarifa kwa kwa njia ya kiufundi.
6.2. Watumiaji wanachukua jukumu kubwa kuhusiana na makala yoyote na michango ambayo wanaanzisha na kutekeleza na wanajitolea kuondoa Gameforge kabisa katika madai au kesi zozote kutoka kwa watu wengine.Huku Gameforge kwa vyovyote vile, ikikosa kudai umiliki wa na michango inayoingizwa na watumiaji,watumiaji wanaipa Gameforge haki ya inayodumu na isiyobadilishwa kutumia makala yaliyomo na michango iliyowekwa nao.Gameforge nayo inasema na kusisitiza kwamba haina mfumo wa kuzingatia na kufuatilia siku zote makala yanayowekwa kwenye kurasa zake.Badala yake,ukaguzi wa ghafla hufanywa na kila mtumiaji ana chaguo la kufahamisha Gameforge kuhusu makala yoyote yasiyokuwa halali na yanayoweza kuvunja sheria husika ambapo Gameforge nayo itaiyikia kwa haraka iwezavyo na kuhariri au kufuta makala hayo yaliyoripotiwa kama inavyohitajika.
6.3. Watumiaji wamepigwa marufuku kuitumia zana yoyote pamoja na hali za mawasiliano zilizopo, lakini si hiyo tu pekee, kwenye kurasa za tovuti ya Gameforge na kuchapiosha au kusambaza yaliyomo hapo ambayo:
a) \thuvunja sheria husika, au tabia zilizopo au viwango vya kimaadili.
b) \thuvunja nembo za watu wengine , sheria, miundo ya viwandani iliyosajiliwa na mengineyo, hakimiliki, siri za biashara au haki za watu wengineo;
c) \tni chafu, ni ya ubaguzi wa rangi, ni ya fujo au ya ufuska kama si ya kuhatarisha maendeleo ya kimaumbile ya watoto na vijana chipukizi;
d) \tni za matusi, unyanyasaji au uchafuliaji jina;
e) \tinahusisha barua za msururu au mifumo ya kilaghai ya kibiashara;
f) \tinasingizia kwa uongo kwamba imewekwa na kuungwa mkono na Gameforge;
g) \tinarejelea deta ya kibinafsi ya watu wengine bila ya idhini yao ya moja kwa moja; au
h) \tni ya kibiashara na/au inatoa huduma ya matangazo.
6.4. Uhusishwaji wa nyavuti, kampuni, au majina ya bidhaa unaruhusiwa tu wakati ambao si kwa sababu ya matangazo ya biashara.
6.5. Watumiaji wote wa hali za mawasiliano zinazotolewa kwenye kurasa za tovuti za Gameforge wanahitajika kuchagua uteuzi unaokubalika wa maneno. Upingaji wa matusi au ushambuliaji wa watu kwa njia isiyofaa utaepukwa.
6.6. Licha ya haki zozote nyingine chini ya masharti haya ya matumizi, Gameforge ina haki ya kubadili na kufuta kabisa au kiasi cha makala hayo yaliyomo na michango, ambayo yanakiuka sheria hizi. Gameforge pia ina haki ya kutowajumlisha watumiaji ambao wanakiuka sheria hizi kwa ukamilifu au kwa kiasi chake katika kutumia zaidi michezo ya mitandaoni,kufikia katika kurasa za nyavuti za Gameforge na huduma nyingine zinazotolewa.
7 Matokeo ya uvunjaji wa jukumu
7.1. Gameforge haitalaumiwa kwa uharibifu unaotokana na uvunjaji wa jukumu unaotokana na mtumiaji.
7.2. Licha ya haki nyingine zozote za kisheria na za utoaji huduma, Gameforge ,kwa uamuzi wake binafsi, inaweza kuchukua hatua zifuatazo kama kutakuwa na idhibati ya watumiaji kukiuka sheria tumikizi , haki za watu wengine, kanuni hizi za matumizi au mahitaji-maalumu yoyote yafaayo ya michezo au sheria.
a) \tkubadili au kufuta makala yaliyomo;
b) \tkutoa onyo kwa mtumiaji;
c) \tuchapisho wa utovu wa nidhamu katika michezo husika ya mtandaoni na kuwatambua watumiaji wanaowajibika.
d)\t uzuiliaji wa muda au wa kabisa wa watumiaji kufikia kwenye michezo yoyote ya mtandaoni na/au ukurasa wa wavuti.
e) \tkutojumlishwa kwa watumiaji;
f) \tutoaji wa marufuku ya muda au ya kabisa katika kuingia kwenye kurasa zote za tovuti ya Gameforge kwenye matukio ya uvunjaji yaliyotajwa katika sehemu ya 6; au
g) \tUsitishwaji wa ghafla wa mikataba ya watumiaji.
7.3. Watumiaji waliozuiliwa au ambao hawajajumlishwa, hawawezi kusajiliwa upya tena bila ya idhini ya mapema kutoka katika kampuni ya Gameforge na wala hawana haki ya kuyafanya marufuku hayo kutojumlishwa, au kuzifanya namna nyingine zozote za marufuku hayo kuondolewa.
8 Ada ya Mtumiaji
8.1. Matumizi ya michezo ya mtandaoni na huduma nyinginezo zinazotolewa hayatozwi chochote, ni bure, mpaka wakati itatajwa vinginevyo.
8.2. Hata hivyo watumiaji wanaweza, kununua baadhi ya huduma zinazotolewa na baadhi ya vipengele vilivyomo kama sehemu ya michezo hiyo ya mtandaoni ambapo watumiaji wataarifiwa ,wao wenyewe kuhusiana na michezo kama hiyo, hali ya vipengele kama hivyo .Hii ni pamoja na kazi zavyo , lakini si tu katika kazi pekee, kipindi cha uwepo, gharama na mbinu za malipo.
8.3. Pale ambapo mtoto anahitaji kununua vipengele fulani vya michezo, anatuhakikishia kwamba yeye amepokea hela hizo za kununua vipengele hivyo vya michezo kutoka kwa walezi wake.
8.4. Malipo yale yaliyokubaliwa huhitajika kulipwa pindi mkataba unapohitimishwa huku yakikusanywa hasa naye yule mtoaji huduma aliyehalalishwa kusimamia mchakato huo wa malipo.Utoaji wa malipo hayo unaweza kufanywa siku chache kabla ili kuhakikisha kutokuwapo kwa huduma hizo.Kanauni na masharti ambayo yanawekwa naye watoaji huduma kama hawa, kama kweli yapo,yanatumika kwa kuongezea Kanuni hizi za matumizi.
8.5. Watumiaji wanahitajiwa kujua kwamba taarifa zozote zilizotolewa kama sehemu ile ya shughuli ya malipo (pamoja na taarifa ya benki, lakini si tu hiyo pekee, nambari ya kadi ya mkopo, n.k.) zinafaa kuwa kweli na sahihi.
8.6. Chaguo la mfumo wa malipo hutofautiana kulingana na mchezo wa mtandaoni, nchi ya mshiriki wa mchezo huo na uwepo wa Mbinu na teknolojia katika mchezo huo.Gameforge inahifadhi haki ya kubadili mbinu za malipo ya michezo hii wakati wowote.
8.7. Gameforge vilevile, inahifadhi haki ya kubadilisha ada za vipengele vya ndani ya mchezo (pamoja na pesa mbalimbali za mtandaoni). Hii ni pamoja na Gameforge kuwa na haki y kupunguza au kuzidisha ada ya vipengele mbalimbali ,vya kibinafi, vya mchezo katika ununuzi wa vipengele hivyo kwenye siku za usoni.
8.8. Endapo kutakuwa na hitilafu ya malipo, riba itakayotozwa ni ileile ya kisheria.Gameforge pia inaruhusiwa kuzuia akaunti ya mtumiaji yeyote ambaye anayo hitilafu ya malipo, kudai kufidia kwa sababu ya uharibifu au kusitisha huduma zake kwa kwa mtumiaji kama huyu.
8.9. Kama ,kwa sababu ya makosa ya mtumiaji, Gameforge itapata kutozwa ada ya kutupiliwa mbali(hundi) (k.m.f kutokana na salio lisilotosha kwenye akaunti) basi, mtumiaji atagharimia gharama hizo zote husika.Gameforge huenda pia ikajumlisha gharama hizi zote na ada wakati itakapokuwa ikimtoza mtumiaji huyo.Endapo malipo yatalipwa kwa kadi ya mkopo, gharama za benkini zinawea kugharimika hadi kiwango cha EUR 50 kwa kila shughuli ya biashara ya kadi ya mkopo pamoja na ada zozote za benkini zilizogharimiwa na Gameforge. Gameforge inaruhusiwa kudai fidia zaidi itakayokuwa imetokana na uharibifu.
9 Kizuizi cha uwajibikaji
9.1. Watumiaji wanawajibika moja kwa moja kwa mtu mwingine endapo watavunja haki zake. Watumiaji hawa wanakubali kwamba watailinda na kuifidia Gameforge dhidi ya uharibifu wote ambao umetokana na kutozingatia majukumu yaliyomo katika kanuni hizi za matumizi. Watumiaji wanaiondoa Gameforge kutoka katika madai yoyote ambayo watumiaji wengine au watu wengine wanaweza kuwa nayo dhidi ya Gameforge kwa uvunjaji wa haki zao kutokana na makala yaliyomo au uvunjaji mwingine wa majukum.Katika hali hii basi watumiaji wanachukua hatua ya kugharimia gharama ya ulinzi wa kisheria wa Gameforge pamoja na gharama zote za mahakama na wakili mradi tu watumiaji waweze kuhusiahwa katika uvunjaji wa sheria hiyo tumikizi.
9.2. Licha ya misingi ya kisheria(Uvunjaji wa jukumu au jambo la utoaji huduma), Uwajibikaji wa Gameforge unategemea kwa ujumla wake mambo yafuatayo:
9.2.1. Mradi tu, Gameforge imetoa huduma ile iliyosababisha uwajibikaji kwa ada ya bure, basi Gameforge itapatikana na utovu wa nia na kuonekana kuwa na uzembe mtupu.
9.2.2. Katika tukio la huduma zilizotolewa ada, Gameforge itawajibika kamilifu kwa utovu wa nia na uzembe kwenye matukio ya jeraha la mwili, Katika tukio la uzembe kiasi basi Uwajibikaji wa Gameforge utazuiliwa kwenye uvunjaji wa majukumu kama haya ya utoaji huduma pamoja na uharibifu na matukio yasiyowezekana na yanayohusishwa na Gameforge.Uwajibikaji wake katika uvunjaji wa majukumu halisi kama haya ya utoaji huduma umezuiliwa katika uharibifu halisi ambao Gameforge ingetarajia katika hitimisho ya mkataba kwa kurejelea maswala ambayo Gameforge ilikuwa na habari nayo wakati huo. “ Majukumu halisi ya utoaji huduma kwa maana yale yaliyojitokeza hapo juu, yanaashiria yale majukumu ambayo ni muhimu sana katika utekelezaji halisi wa mkataba huu na utambuzi wa mada yake na yanategemewa kwa kiasi fulani na watumiaji”
9.2.3. Gameforge haitachukulia uwajibikaji wowote kwa usumbufu ambao haikusababisha ndani ya mtandao.
9.2.4. Kwa kuzingatia aya zinazofuata, uwajibikaji wa Gameforge katika upotezaji wa deta, utakuwapo tu kama upotezaji huo usingezuilika na watumiaji hao kupitia kwa mbinu za makini na usalama –wa-deata.
9.2.5. Vizuizi vya uwajibikaji vilivyotajwa hapo juu, havitumiki kwenye matukio ambayo(i)Gameforge ilitoa udhamini na uhakikisho halisi,(ii)ni uwongo (iii) ni uharibifu kutokana na majeraha kwa maisha,mwili au afya na (iv) sheria tumikizi inakariri vinginevyo.
10 Kipindi cha mkataba; ufutaji wa akaunti za mtumiaji
10.1. Pengine kama kauli itatolewa kuhusiana na mchezo au huduma ya mtandaoni, mkataba utakaotumika kwenye Kiingilio cha Gameforge na kwenye michezo ya mtandaoni na huduma nyinginezo zinazotolewa ni kwa kipindi kisichojulikana na kipindi hicho kinaanza wakati ule wa usajili au kupokelewa na Gameforge.
10.2. Hata bila ya sababu nzuri ,mkataba unaweza kusitishwa na kundi lolote lile wakati wowote na tena mara moja, mradi tu hakuna kipindi maalumu cha mkataba kisiwe kimekubaliwa. Endapo kipindi cha muda cha mkataba kimekubaliwa kati ya makundi hayo basi mkataba utasitishwa tu kamilifu kwenye mwisho wa kipindi hicho.Endapo na mpaka mkataba huo utakapositishwa, basi inachuliwa kwamba mkataba huo utakuwa ukirefushwa kiatomatiki kwa kipindi kile cha mkataba kilichokubaliwa awali.
10.3. Kila kundi lina haki ya kusitisha mkataba bila ya kutoa arifa kwa sababu mbalimbali nzuri. Sababu muhimu itakayofanya haya kufanyika ni ikiwa na endapo:
a) \twatumiaji hawalipi malipo waliotozwa, na hawayalipi licha ya kumbusho;
b) \twatumiaji wanajihusisha katika tabia ambayo inaathiri uchezwaji wa mchezo na wachezaji wengine pakubwa;
c) \tudanganyifu, modi na/au “utapeli” au viinieroro vinginevyo, zana, au miswada inayotumiwa katika kubadili na furaha na/au mfumo wa uchezwaji wa michezo ya mtandaoni;
d) \takaunti ya mtumiaji mwingine inatumiwa na makundi mengine , isipokuwa tu kama sheria ya mchezo inatoa maelekezo kama hayo.
e) \twatumiaji wanachezea kwenye akaunti za mtumiaji mwingine au wanatumia zaidi ya akaunti moja ya mtumiaji katika kila mchezo wa mtandaoni. , isipokuwa tu kama sheria ya mchezo inatoa maelekezo kama hayo.
f) \twatumiaji wanavitumia vifaa vya mtandaoni vinavyotumiwa kwenye michezo ya mtandaoni, nje ya michezo hiyo ya mtandaoni, au wanajaribu kubadilishana au kuuza kwa hela “halisi”; au
g) \twatumiaji kwa kutowajibika wanazivunja sheria tumikizi, kanuni hizi za matumizi au mahitaji-maalumu ya michezo au sheria.
10.4. Arifa ya usitisho lazima itolewe kwa maandishi , baruameme ikiwa ndiyo mbinu inayokubalika katika mawasiliano ya maandishi.
10.5. Ndani ya kuwepo kwa sababu nzuri (k.m.f. kipindi kilichorefushwa bila shughuli za kazi), Gameforge inaruhusiwa kufutilia mbali akaunti za mtumiaji. Aidha Gameforge inaweza, kwa chaguo lake, kuzifuta akaunti za mtumiaji pindi mwisho wa mkataba uhikapo.
11 Ufaragha
11.1. Deta ya kibinafsi ya mtumiaji haiwekwi pamoja, wala kupitishwa kwenye mchakato au kutumiwa mpaka wakati ambao mtumiaji husika amekubali au sheria tumikizi (k.m.f., sheria ya ulinzi wa deta ya Ujerumani (Bundesdatenschutzgesetz) au sheria ya vyombo vya habari na mawasiliano( Telemediengesetz)) inaelekeza hivyo au kuruhusu.
11.2. Kwa maelezo zaidi, tazama Kauli ya ufaragha ya Gameforge.
12 Sheria Tumikizi ,mahali pa Kisheria
12.1. Sheria za shirikisho la Jamuhuri ya Ujerumani zinatumika, bila ya kuorodhesha CISG yani Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kandarasi za Uuzaji wa Kimataifa wa bidhaa.
12.2. Kwa watumiaji ambao hawako kwenye mamlaka ya mahakama ya Ujerumani, au wao ni mfanyabiashara (Kaufmann) kwa mujibu wa maana ya kijerumani msimbo wa kibiashara (Handelsgesetzbuch), mahali pa kisheria ni pale ambapo afisi za Gameforge zilizosajiliwa zipo.Pamoja na hayo Gameforge inaruhusiwa kushatki hata katika mahali pa kisheria pa watumiaji.
13 Marekebisho ya Kanuni hizi za matumizi, mengineyo, mawasiliano, kauli kimbizi
13.1. Gameforge inayo haki ya kurekebisha kanuni hizi za matumizi.Wakati wa kuingia kwenye akaunti, watumiaji wanaarifiwa kuhusu marekebisho yaliyofanyiwa kanuni hizo za matumizi kwenye kiingilio cha Gameforge au kwenye ukurasa wowote wa mchezo wa mtandaoni ndani ya kipindi kisichopungua wiki mbili kabla ya kutekelezwa kwa marekebisho hayo.Vilevile Gameforge huenda ikaarifu watumiaji kupitia kwa baruameme ama kwa marekebisho hayo ya kanuni au kwa kuwa na kiungo kitakachounganishwa kwenye wavuti wa Gameforge ambapo kanuni hizo zilizorekebishwa zinaweza kuonekana. Kwa kuingia kwenye kiingilio cha Gameforge au kwenye mchezo wowote wa mtandaoni baad aya kutekelezwa kwa kanuni hizo zilizorekebishwa,watumiaji wajieleza jinsi ambavyo wanakubaliana na kanuni hizo mpya.Gameforge itawashauri watumiaji binafsi kuhusu umuhimu wa kipindi kile cha wiki mbili,haki ya ufutiliaji mbali wa kanuni hizo mpya na athari za kisheria endapo wao wataamua kutochukulia hatua yoyote kanuni hizo lakini kwa njia ifaayo.
13.2. Watumiaji hawawezi kuhamisha haki na majukumu yao kwenye mkataba huu kabla ya idhini kwa maandishi kutoka kwa Gameforge.
13.3. Watumiaji wanaruhusiwa tu kuanza kudai marekebisho hayo ya kanuni, pale ambapo na kwa kiwango ambachomadai hayo yameeleweka na kutambuliwa kikamilifu na Gameforge au hayajapingwa.Watumiaji wanaweza kufurahia haki ya kubakiza endapo tu madai haya yatathibitishwa.
13.4. Pengine tu kama Kanuni hizi za Matumizi zitakariri vinginevyo,Gameforge kwa hakika,huwasiliana na watumiaji kwa baruameme.Ni jukumu la watumiaji wa wakati huo kuhakikisha kuwa baruameme iliyotolewa wakati wa usajili katika kampuni ya Gameforge inaangaliwaangaliwa mara kwa mara ili kuona kama kunao ujumbe wowote kutoka Gameforge. Wakati anawasiliana na Gameforge, watumiaji lazima waonyeshe ni (m)michezo ipi ya mtandaoni waliyocheza na ni akaunti gani ya mtumiaji walitumia.
13.5. Mabadiliko yoyote na uhairisho wa kanuni hizi za matumizi, pamoja na sharti hili la kirasmi, lazima liwasilishwe kwa maandishi.
13.6. Endapo kauli zozote kwenye kanuni hizi za matumizi ni au haziwezi kutumika au zinavunja sheria tumikizi basi kauli zinazosalia kwenye kanuni za matumizi, zitaendelea kutumika kwa nguvu na athari, na makundi hayo yatachukua kauli hizo zisizotumika na kuzibadilisha na zile ambazo zinakaribiana bora zaidi na maana ya kiuchumi na kusudio la kauli hizo zisizotumika ndani ya mipaka ya kisheria.Hayo pia ni kweli katika mapengo yatakayopatikana hapa.


Karlsruhe, January 15, 2009

Gameforge Productions GmbH
Albert-Nestler-Strasse 8
76131 Karlsruhe
Germany

Local Court Mannheim, Commercial Register Number: HRB 701682
Sales Tax Identification Number: DE254298652
CEO: Alexander Rösner


Navigation:

 -  Terms of Use Gameforge Productions GmbH - 
 - Gameforge Productions GmbH legal notice - 
 - Gameforge Productions GmbH Privacy Statement -